Walimu wamekubaliana kwamba mwaka mpya wa masomo 2026 – 2027 utakuwa ni mwaka wa ubunifu na marekebisho ya kimbinu, ili kuhakikisha wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) wanapata elimu ya kina ya sekula na elimu ya Hawza kwa uwiano bora, bila upande mmoja kuathiriwa na mwingine.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Walimu wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania wamefanya kikao muhimu kwa ajili ya kujadili na kuweka mfumo mpya na bora zaidi wa masomo ya QT (sekula) na masomo ya Hawza kwa wanafunzi wa taasisi hiyo katika muhula mpya wa masomo wa mwaka 2026 – 2027.
Katika kikao hicho, masuala kadhaa yamejadiliwa kwa kina, ikiwemo:
Ratiba shirikishi ya masomo ya QT na Hawza ili kuepusha mgongano wa muda na kuhakikisha mwanafunzi anaendelea vyema katika pande zote mbili.
Mbinu za tathmini na mitihani ya kila wiki, ili kuhakikisha wanafunzi wanapimwa mara kwa mara na kupewa mrejesho wa kielimu.
Uimarishaji wa nidhamu ya kielimu na kiroho, ili elimu ya QT na Hawza iende sambamba na malezi bora ya kimaadili na kiimani.
Ushirikiano kati ya walimu wa QT na Hawza kwa lengo la kusaidiana katika malezi ya wanafunzi na kufuatilia maendeleo yao ya kielimu na kitabia.

Your Comment